• HABARI MPYA

  Saturday, May 05, 2018

  FERGUSON APATWA UGONJWA WA AKILI, AKIMBIZWA HOSPITALI KWA MATIBABU

  KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amekwenda kufanyiwa upasuaji wa ubongo baada ya hofu juu ya maisha yake.
  Gari la wagonjwa lilimbeba babu huyo wa umri wa miaka 76 kutoka nyumbani kwake, Cheshire mida ya Saa 3 asubuhi ya leo na kumpeleka hospitali ya Macclesfield.
  Mscotland huyo alikimbizwa hospitali kwa kusindikizwa na msafara wa Polisi ili kwenda kutibiwa Salford Royal.
  Taarifa ya Manchester United imesema; "Sir Alex Ferguson amekwenda kufanyiwa upasuaji wa dharula leo kutokana na matatizo ya kuharibika kwa ubongo wake,".
  "Taratibu zimekwenda vizuri sana, lakini anahitaji kipindi kikubwa cha uangalizi makini ili apate ahueni vizuri. Famili yake imeomba faragha katika jambo hili,".
  Wachezaji wa Manchester United walikuwa wakisikilzia juu ya hali ya Ferguson kabla ya klabu kutoa taarifa rasmi juu yake. 
  Sir Alex Ferguson amekwenda kufanyiwa upasuaji wa ubongo kutokana na hofu iliyoibuka juu ya maisha yake

  Ferguson alikuwepo Uwanja wa Old Trafford mwishoni mwa wiki iliyopita klabu yake ya zamani ikimenyana na Arsenal katika mchezo wa mwisho wa Arsene Wenger dhidi ya wapinzani wake wa muda mrefu.
  Ferguson alikwenda uwanjani kumkabidhi zawadi Wenger kutoka klabuni akiwa sambamba na kocha wa sasa wa United, Mourinho.
  Mscotland huyo anafahamika kwa mafanikio yake makubwa enzi zake akiwa kocha wa Manchester United akibeba mataji zaidi ya 27 na kujijengea heshima kubwa kwenye soka ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FERGUSON APATWA UGONJWA WA AKILI, AKIMBIZWA HOSPITALI KWA MATIBABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top