TIMU ya Ufaransa imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sweden usiku wa jana Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, Bergen County, New Jersey, Marekani.
Mabao ya Les Bleus yamefungwa na washambuliaji, Kylian Mbappé Lottin wa Real Madrid ya Hispania mwenye asili ya Cameroon, mawili dakika ya 45 na 74 na Bradley Jean-Manuel Essolisam Addo wa Paris Saint-Germain ya kwao, mwenye asili ya Togo dakika ya 53.



.png)
0 comments:
Post a Comment