• HABARI MPYA

    Saturday, July 04, 2026

    NI SIMBA SC WASHINDI WA KOMBE LA CRDB, AZAM YALALA 1-0 PEMBA


    TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
    Ilikuwa siku mbaya kwa kiungo Yayha Zayd Omar aliyejifunga dakika ya 61 akijaribu kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa na winga Elie Mpanzu Kibisawala, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Ikawa siku mbaya zaidi kwa Azam FC baada ya kiungo wake tegemeo, Feisal Salum Abdallah kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya baada ya purukushani ya kawaida na winga Msenegal, Libasse Guèye.

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI SIMBA SC WASHINDI WA KOMBE LA CRDB, AZAM YALALA 1-0 PEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top