TIMU ya Misri imefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na Australia ndani ya dakika 120 usiku huu Uwanja wa AT&T Jijijni Arlington, Texas, nchini Marekani.
Mabao yote yamefungwa na wachezaji wa Al Ahly ya Cairo, kiungo Emam Ashour Metwally Abdel Ghany akianza kuifungia Misri dakika ya 13, kabla ya beki wa kulia, Mohamed Hany Gamal El-Demerdash kujifunga dakika ya 55 kuipatia Australia bao la kusawazisha.
Katika mikwaju ya penalti waliofunga za Mafarao wa Misri ni kiungo Mahmoud Saber Abdelmohsen Hassan Abdelmohsen anayecheza kwa mkopo ZED kutoka Pyramids zote za kwao, beki Ramy Hisham Abdel Aziz Mostafa Rabia wa Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE), aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah Hamed Mahrous Ghaly na beki wa Zamalek ya Cairo, Hossam Abdelmageed Abdelsalam Abdelmegeed.
Upande wa Australia mabeki Harry James Souttar wa Leicester City ya England mzaliwa wa Scotland na pacha wake, Lucas Herrington wa Colorado Rapids ya Marekani mwenye asili ya Zimbabwe wote walipiga juu ya lango.
Waliofunga penalty za Kangaroo ni kiungo wa FC St. Pauli ya Ujerumani, Jackson Alexander Irvine na winga wa CD Castellón ya Hispania, Awer Bul Mabil aliyezaliwa kwenye kambi ya Wakimbizi nchini Kenya, wazazi wake wakitokea Sudan Kusini.



.png)
0 comments:
Post a Comment