UBELGIJI imetoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Senegal katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 kufuatia timu hizo kufungana 2-2 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Lumen Field, Seattle, Washington, Marekani.
Senegal ilitangulia kwa mabao ya nyota wake wanaocheza England, kiungo Mouhamadou Habib Mbacke Diarra wa Sunderland dakika ya 25 na na mshambuliaji Ismaïla Sarr wa Crystal Palace dakika ya 51.
Lakini Ubelgiiji ikatoka nyuma kwa mabao ya wachezaji wake wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mshambuliaji wa Napoli ya Italia, Romelu Lukaku Bolingoli dakika ya 86 na kiungo wa Aston Villa ya England, Youri Marion Achiel Tielemans mawili dakika ya 89 na la penalti dakika ya 120’+5.



.png)
0 comments:
Post a Comment