MABINGWA watetezi, Argentina wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Misri usiku huu Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia, Marekani.
Mafarao wa Misri walitangulia kwa mabao ya wachezaji wake wanaocheza ligi ya nyumbani. beki wa kati, Yasser Ibrahim Ahmed El Hanafi wa Al Ahly dakika ya 15 na winga wa kushoto, Mostafa Mohamed Zaky Abdelraouf ‘Zico’ wa Pyramids dakika ya 67.
Argentina ikazinduka kwa mabao ya beki wa kati wa Tottenham Hotspur ya England, Cristian Gabriel Romero dakika ya 79, mshambuliaji, Lionel Andrés Messi wa Inter Miami ya Marekani dakika ya 83 na kiungo, Enzo Jeremías Fernández wa Chelsea ya England dakika ya 90’+2.
Mapema dakika ya 21 Lionel Messi alikosa penalti baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Al Ahly ya Misri, Mostafa Shobeir na sasa Argentina watakutana na mshindi kati ya Uswisi na Colombia zitakazomenyana baadaye usiku huu Uwanja wa BC Place, Vancouver nchini Canada.



.png)
0 comments:
Post a Comment