// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 20, 2014

    NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    KIKOSI cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes chenye watu 25 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).
    Mechi hiyo itachezwa Jumamosi Mei 24 mwaka huu katika Jiji la Kaduna kwenye Jimbo la Kaduna ambalo lipo katikati ya Nigeria. Msafara wa timu hiyo unaoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi unaondoka kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
    Ngorongoro Heroes inayonolewa na Kocha John Simkoko ilipoteza mechi ya kwanza iliyofanyika nyumbani jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-0.
    Kikosi cha Ngorongoro kilichofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza na Nigeria Dar es Salaam

    Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat wa Tchad ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Atasaidiwa na Issa Yaya, Alfred Madjihoudel na Idriss Biani wote kutoka Tchad. Kamishna ni Aboubakar Alim Konate wa Cameroon.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAENDA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top