// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSHAHARA WA VAN GAAL HUU HAPA NA ANAPEWA PAUNI MILIONI 200 ZA USAJILI...ATAKA KUUNDA 'TIMU LA DUNIA' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSHAHARA WA VAN GAAL HUU HAPA NA ANAPEWA PAUNI MILIONI 200 ZA USAJILI...ATAKA KUUNDA 'TIMU LA DUNIA' - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 20, 2014

    MSHAHARA WA VAN GAAL HUU HAPA NA ANAPEWA PAUNI MILIONI 200 ZA USAJILI...ATAKA KUUNDA 'TIMU LA DUNIA'

    KOCHA Louis van Gaal atakuwa analipwa mshahara wa Pauni Milioni 6 kwa mwaka na atapewa Pauni Milioni 200 kwa ajili ya kufanya usajili wa maana Manchester United.
    Kocha huyo Mholanzi aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya David Moyes, amesaini Mkataba wa miaka mitatu na kutangazwa rasmi mchana wa jana na atakuwa anasaidiwa na Ryan Giggs.
    Klabu bado inataka kujumuisha watu watatu wa Class of 92 katika bench la Ufundi, Phil Neville, Nicky Butt na Paul Scholes -lakini bado hakuna uamuzi uliotolewa hadj sasa.
    Van Gaal ataanza kazi rasmi baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao nchini Brazil ambako ataiongoza Uholanzi kwa mara ya mwisho.
    Van Gaal anataka kuwasajili mabeki Wajerumani Mats Hummels na Holger Badstuber, viungo Toni Kroos na Arjen Robben na mshambuliaji Mario Mandzukic kuimarisha Man United ya kushindani mataji msimu ujao.
    Kocha mpya: Louis van Gaal atapewa Pauni Milioni 200 za kufanyia usajili Manchester United
    WANAOTAKIWA NA VAN GAAL...
    KEVIN STROOTMAN 
    Roma Pauni Milioni 25, miaka 24
    2013-14 mechi: 28  mabao: 6
    Anatumia mguu wa kushoto, mtaalamu, lakini hana kasi. Anasumbuliwa na maumivu goto na hataweza kuingia uwanjani hadi Oktoba.
    CESC FABREGAS 
    Barcelona Pauni Milioni 45, miaka 27
    2013-14 Mechi: 55  Mabao: 13
    Anauzwa. United inaweza kujaribu bahati yake.
    TONI KROOS 
    Bayern Munich Pauni Milioni 18, miaka 24
    2013-14 Mechi: 51  Mabao: 4
    Alikubali kujiunga na timu chini ya David Moyes. Van Gaal bado analitamani zao hilo la akademi ya Munich.
    MATS HUMMELS 
    Borussia Dortmund Pauni Milioni 20, miaka 25
    2013-14 Mechi: 28  Mabao: 2
    Hayuko fiti sana  lakini ni beki la kazi. Dortmund inaweza kumuuza
    HOLGER BADSTUBER 
    Bayern Munich Pauni Milioni 15, miaka 25
    2013-14 Hajacheza mechi hata moja, lakini mbele ya van Gaal huyo ndiye beki bora zaidi anayetumia mguu wa kuhsoto ndani ya Ujerumani.
    LUKE SHAW 
    Southampton Pauni Milioni 27, miaka 18
    2013-14 Mechi : 36  Hajafunga bao
    Mchezaji huyo wa kimataifa wa England anaweza kujiunga na United mara sakata la ada ya uhamisho wake litakapomalizwa.
    SEBASTIAN JUNG 
    Eintracht Frankfurt Pauni Milioni 7, miaka 23
    2013-14 Mechi: 36     Bao: 1
    Beki wa kulia wa pili bora Ujerumani baada ya Philipp Lahm, ambaye Arsenal pia wanamtaka.
    (Imeandaliwa na Simon Jones)Winged wonder: Bayern Munich star Arjen Robben is being considered by his national manager as a target
    Winga teleza: Nyota wa Bayern Munich, Arjen Robben naye anatakiwa kocha van Gaal, ambaye pia ni kocha wake Uholanzi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSHAHARA WA VAN GAAL HUU HAPA NA ANAPEWA PAUNI MILIONI 200 ZA USAJILI...ATAKA KUUNDA 'TIMU LA DUNIA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top