UGANDA YAPIGWA 2-1 NA MADAGASCAR MBIO ZA Na Nurat Mahmoud, Madagascar
UGANDA imefungwa mabao 2-1 na Madagascar katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 Morocco.
Lakini sifa zimuendee mshambuliaji wa Yanga SC ya Tanzania, Hamisi Kiiza ‘Diego’ aliyeifungia The Cranes bao muhimu la ugenini.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Fabrice Rakotondraibe aliyefunga kwa penalti dakika ya tisa baada ya kufanyiwa faulo kwenye eneo la hatari na Henry Kalungi.
Wenyeji walipata bao la ushindi dakika ya 29, baada ya Njiva Rakotoharimalala kumtoka beki wa kushoto Ochaya na kufunga.
Kocha wa Cranes, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic aliwaingiza Francis Olaki na Brian Majwega kuchukua nafasi za Martin Mutumba na Hassan Wasswa ambao walikwenda kubadilisha mchezo.
Lakini wenyeji walipata penalti nyingine, baada ya pasi ya kurudisha kwa kichwa kwa kipa ya Guma kutomfikia kipa Wetanga, ambaye alitoka langoni mwake na kwenda kumfayia faulo mshambuliaji wa Madagascar.
Kipa wa Uganda alikuwa na bahati kwa kuonyeshwa kadi ya njano tu na Cranes wakapata nafasi nyingine baada ya mpigani wa penalti ya Madagascar kupaisha juu ya lango.
Cranes, ambayo baadaye ilimuingiza mshambuliaji Daniel Sserunkuma kuchukua nafasi ya Ochaya dakika za mwishoni ilipata penalti baada ya beki wa Madagascar, Tobisoa Njakanirina kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na Kiiza akaenda kufunga.
Uganda sasa itahitaji ushindi japo wa 1-0 katika mchezo wa marudiano mjini Kampala wikiendi ijayo ili kusonga mbele.

![]() |
| Hamisi Kiiza ameifungia Uganda bao muhimu la ugenini |

.png)
0 comments:
Post a Comment