Na Prince Akbar, Abidjan
TIMU ya Sewe Sport ya Ivory Coast imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika jana Uwanja wa Robert Champroux.
Wenyeji walitawala mchezo kipindi cha kwanza na wakapata bao la kuongoza kupitia kwa Herman Kouao dakika ya 30 aliyekutana na pasi ya Roger Assale na kufumua shuti lililombabatiza beki wa Etoile kabla ya kutinga nyavuni.
Pamoja na hayo, timu ya kocha Roger Lemerre ilizinduka kipindi cha pili na kupata kile walichokifuata Ivory Coast.
Marouane Tej na Issam Jebali walikaribia kufunga dakika ya 60, lakini alikuwa ni Baghdad Bounedjah aliyeifungia timu yake bao la kusawazisha dakika ya 79.
Vinara wa Kundi B ni Al Ahly, ambao waliifunga Nkana FC ya Zambia, huku Etoile du Sahel na Sewe zikiwafuatia vigogo hao wa Misri kila timu ikiwa na pointi moja.
‘Sewekes’ itasafiri hadi Zambia wikiendi ijayo, wakati Etoile Sportive du Sahel itakuwa mwenyeji wa Mashetani Wekundu wa Cairo katika mechi za pili za kundi hilo.

![]() |
Sewe Sport imelazimishwa sare na Etoile du Sahel nyumbani |
Marouane Tej na Issam Jebali walikaribia kufunga dakika ya 60, lakini alikuwa ni Baghdad Bounedjah aliyeifungia timu yake bao la kusawazisha dakika ya 79.
Vinara wa Kundi B ni Al Ahly, ambao waliifunga Nkana FC ya Zambia, huku Etoile du Sahel na Sewe zikiwafuatia vigogo hao wa Misri kila timu ikiwa na pointi moja.
‘Sewekes’ itasafiri hadi Zambia wikiendi ijayo, wakati Etoile Sportive du Sahel itakuwa mwenyeji wa Mashetani Wekundu wa Cairo katika mechi za pili za kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment