// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBEYA CITY WAKWAMA KWENDA SUDAN KISA CECAFA HAIJATUMA TIKETI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBEYA CITY WAKWAMA KWENDA SUDAN KISA CECAFA HAIJATUMA TIKETI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2014

    MBEYA CITY WAKWAMA KWENDA SUDAN KISA CECAFA HAIJATUMA TIKETI

    Na Samira Said, Dar es Salaam
    KIKOSI cha timu ya Mbeya City cha jijini Mbeya jana kilishindwa kuondoka nchini kuelekea Sudan kushiriki mashindano ya Kombe na Nile Basin kutokana na tiketi za ndege kutokuwepo.
    Mbeya City imepata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya Azam kuikacha michuano hiyo ikieleza kwamba kwa sasa wachezaji wake wako likizo.
    Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, aliiambia BIN ZUBEIRY kuwa bado hawajajua kikosi chao kitasafiri lini.
    Kimbe alisema wachezaji 20 wa timu hiyo watawasili jijini Dar es Salaam leo Jumatatu asubuhi wakisubiri tiketi za kuelekea Sudan.

    “Tulikubaliana awali timu yetu iondoke nchini Jumapili ili tupate muda wa kuzoea hali ya hewa, ila hadi leo  (Jumapili jioni ) tiketi hazijatumwa, TFF inaendelea na mawasiliano na CECAFA", alisema Kimbe.
    Aliongeza kuwa wameona ni bora waje Dar es Salaam kuendelea na mazoezi na kusubiria safari hiyo wakiwa jijini.
    "Timu ilianza mazoezi mapema na huko tutaenda kushindana na kuonyesha uwezo wetu na changamoto kama ilivyokuwa katika ligi", Kimbe aliongeza.
    Alisema pia maandalizi yao yatawapa wachezaji wao uzoefu wa kimataifa na kuahidi kwamba msimu ujao Mbeya City itakuwa moto zaidi.
    Katika ligi ya Bara Mbeya City ilimaliza ikiwa ya tatu nyuma ya bingwa Azam na Yanga walioshika nafasi ya pili.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY WAKWAMA KWENDA SUDAN KISA CECAFA HAIJATUMA TIKETI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top