Na Prince Akbar, Blantyre
MABAO mawili ya Frank ‘Gabadinho’ Mhango jana yameipa Malawi ‘The Flames’ ushindi wa 2-0 dhidi ya Chad katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015 Morocco uliofanyika Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre.
Mshambuliaji huyo wa Bloemfontein Celtic, ambaye anatarajiwa kushinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), aliifungia The Flames bao la kwanza dakika ya tano.
Alifunga bao hilo akimtungua kipa wa Chad Dillah Mbiramadji kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Joseph Kamwendo. Alifunga bao la pili dakika ya 73 baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Chad katika kuukimbilia mpira mrefu, ambao alipoufikia alikimbia nao kabla ya kufunga.
Malawi sasa itasafiri kuifuata Chad wikiendi ya Mei 30 kwa ajili ya mchezo wa marudiano na mshindi wa jumla atamenyana na ama Sao Tome au Benin kuwania kupangwa kwenye kundi.
Kikosi cha Malawi jana kilikuwa: Charles Swini, Harry Nyirenda, Moses Chavula Bashir Maunde, John Lanjesi, Joseph Kamwendo, Chimango Kayira, Rodrick Gonani/Frank Banda, John Banda/Micium Mhone, Frank ‘Gabadinho’ Mhango na Atusaye Nyondo.
Chad: Dillah Mbiramadji, Hussein Hassan, Massama Aikiliout, Kelvin Jatita, Morgan Betorangal, Mahamati Yassi, Hiraire Kedgui, Leger Djimeanan/Casmir Rodrigues, Marius Mbaima, Sylvian Ididanger/Karl Max Dany na Ezecheir Dousrl.
Katika mechi nyingine za jana za hatua hiyo ya mbio za Morocco 2015, Sao Tome e Principe ilifungwa 2-0 nyumbani na Benin, Namibia iliilaza 1-0 Kongo na Mauritania iliibwaga 1-0 Equatorial Guinea.
Mechi nyingine za mchujo zinatarajiwa kuendelea leo, mjini Dar es Salaam, wenyeji Tanzania wakiikaribisha Zimbabwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Guinea Bissau, Swaziland vs Sierra Leone, Msumbiji vs Sudan Kusini, Madagascar vs Uganda, Burundi vs Botswana, Liberia vs Lesotho, Kenya vs Comoros na Libya vs Rwanda.

![]() |
| Mshindi wa mechi; Frank 'Gabadinho' Mhango jana ameifungia mabao yote Malawi ikishinda 2-0 dhidi ya Chad |

.png)
0 comments:
Post a Comment