• HABARI MPYA

    Friday, July 13, 2012

    SAFU YA UONGOZI YANGA HII HAPA, KASWAHILI AIPIGA ZENGWE

    Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili ameonya juu ya kampeni chafu kuelekea uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika Jumapili, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Akizungumza makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kaswahili amesema hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa, ikiwemo watu kufutiwa uanachama. Miongoni mwa aliyokemea ni vipeperushi vinavyoonyesha safu kamili ya watu wa kuwachagua kwenye uchaguzi huo. Pichani Kaswahili akionyesha kipeperushi chenye safu ya uongozi iliyopangwa.

    Safu ya uongozi iliyokemewa na Kaswahili, lakini si inafaa kabisa hii jamani? 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAFU YA UONGOZI YANGA HII HAPA, KASWAHILI AIPIGA ZENGWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top