• HABARI MPYA

    Saturday, July 28, 2012

    NIZAR APONA KWA NGUVU ZA MUNGU, KUWAVAA AZAM


    Nizar Khalfan

    Na Prince Akbar
    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyesajiliwa na Yanga msimu huu, ambaye awali ilielezwa atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita baada ya kuumia nyonga, amepona kwa ‘Nguvu za Mungu’ na ameorodheshwa kwenye Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inayotarajiwa kaunza saa 10:00 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
    Meneja wa Yanga, Hafidh Suleiman ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba, Nizar amepona na ataanzia benchi kwenye mechi ya leo dhidi ya Azam.
    Mapema jana, kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba Nizar alionyesha dalili za kupona mapema awali, lakini sasa imegundulika anatakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki zisizopungua sita.
    Kwa masikitiko makubwa, Tom alisema; “Nizar hatacheza fainali, alionekana kuwa vizuri siku chache zilizopita, sasa atakuwa nje kwa wiki zisizopungua sita,”alisema.
    Tayari Nizar amekosa mechi mbili za Robo Fainali na Nusu Fainali ya michuano hiyo, licha ya kuanza vizuri katika hatua ya makundi. Kiungo huyo alisajiliwa na Yanga miezi miwili iliyopita akitokea Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), ambayo alijiunga nayo kutoka Vancouver Whitecaps ya Canada, ambayo ilikuwa inacheza MLS.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIZAR APONA KWA NGUVU ZA MUNGU, KUWAVAA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top