• HABARI MPYA

    Saturday, July 28, 2012

    AS VITA WA TATU KAGAME, YANGA NA AZAM NYASI ZINAIPATA FRESH HIVI SASA


    Kikosi cha Yanga leo


    Kikosi cha Azam leo
    Na Prince Akbar
    FAINALI ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, kati ya Yanga SC na Azam FC inaendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiifunga 2-1 APR ya Rwanda.
    Mechi kati ya Yanga na Azam inachezeshwa na refa Thierry Nkurunzinza kutoka Burundi, akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na Peter Sabatia wa Kenya, wakati mezani atakaa Issa Kagabo wa Rwanda, Kamisaa Hassan Amir wa Somalia na Mtathmini wa marefa ni Anangwe Robert wa Kenya. 
    Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende. Benchi; Shamte Ally, Juma Seif, Ladislaus Mbogo, Idrisa Assenga na Jerry Tegete.
    Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Jabir Aziz, Kipre Tcheche, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’. Benchi; Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.
    Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao yake yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67, wakati la kufutia machozi la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa na Jean Mugiraneza dakika ya 89.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AS VITA WA TATU KAGAME, YANGA NA AZAM NYASI ZINAIPATA FRESH HIVI SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top