Mshambuliaji wa Atleticon ya Burundi, Didier Kavumbangu (pichani) amesaini Yanga juzi. Kiongozi Mkuu wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Ahmad 'Magari' ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wamemsajili mchezaji huyo na sasa wameimarisha safu yao ya ushambuliaji, yenye wakali wengine kama Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi. Kavumbangu ndiye aliyefunga mabao yote mawili katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, Yanga ikilala 2-0 mbele ya Atletico, mchezo pekee mabingwa hao wa Kagame kufungwa mashindano ya mwaka huu. |
0 comments:
Post a Comment