• HABARI MPYA

    Thursday, July 19, 2012

    MEDDIE KAGERE AWAACHA SOLEMBA YANGA, ATIMKIA AFRIKA KUSINI

    photo
    Kagere hapa katika mechi kati ya Rwanda na Benin


    MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Rwanda, Meddie Kagere jana alitarajiwa kuondoka nchini humo kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya nchini humo, Bidvest Wits Football Club.
    Kagere, anayetajwa kutakiwa na Yanga, alizungumza na gazeti la Times la Rwanda na kusema, “Natakiwa kwenda Afrika Kusini leo (jana) kufanya majaribio Bidvest Wits FC,”
    “NItakuwa huko kwa mwezi mmoja na ikiwa mambo yatakwenda vizuri, wakati utaamua kama nitajiunga na klabu hiyo au la,”
    “Ikiwa mambo hayatakwenda vizuri Bidvest Wits FC, nitakwenda kufanya majaribio klabu nyingine, ambazo Meneja wangu hajazithibitisha hadi sasa hadi sasa,” alisema mchezaji huyo wa zamani wa Mukura na SC Kiyovu.
    Kocha  Mkuu wa Amavubi, Milutin Sredojovic 'Micho' ambaye yuko katika jitihada kubwa za kuinua soka ya Rwanda’, yuko Ulaya tangu mwezi uliopita kusaka klabu kwa ajili ya wachezaji wa  APR, Jean Baptiste Mugiraneza, Jean Claude Iranzi na Olivier Karekezi.
    Kagere, ambaye amekuwa tegemeo la Amavubi na klabu yake, Polisie, alitarajiwa kujiunga na klabu moja ya Saudi Arabia, lakini dili lilikufa kutokana na mawasiliano duni.
    Mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 26, ameichezea kwa misimu miwili Polisi, akiifungia mabao 28 katika misimu miwili ya Ligi Kuu.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Atraco, pia ana ofa kutoka klabu za  Yanga, Gor Mahia ya Kenya, APR na St. George ya Ethiopia.
    Kagere anatarajiwa kuungana na beki mzaliwa wa Uganda, Timothy Batabaire, ambaye ni mchezaji tegemeo wa klabu hiyo, ambayo ilimaliza katika nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MEDDIE KAGERE AWAACHA SOLEMBA YANGA, ATIMKIA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top