• HABARI MPYA

    Thursday, July 19, 2012

    COASTAL UNION YATINGA FAINALI BURUNDI


    Na Prince Akbar
    TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Coastal Union ya Tanga, leo imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Rollingston, baada ya kuwafunga mabingwa watetezi, Ruvu Shooting mabao 2-1 nchini Burundi.
    Mabao yote ya Coastal yalitiwa kimiani na Mohamed Miraj, wakati bao la Ruvu waliotwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka jana mjini Arusha, lilitiwa kimiani na Said Hussein.
    Kwa matokeo hayo, Coastal itamenyana na Ecofoot ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo katika Nusu Fainali nyingine leo, waliitoa Mjini Magharibi ya Zanzibar kwa mabao 2-1 pia.
    Mabao ya Ecofoot yalitiwa kimiani na Sais Kabamba na Shukuru Hamisi, wakati bao la kufutia machozi la Mjini Magharibi lilitiwa kimiani na Omar Tamim. Sasa, Mjini Magharibi itamenyana na Ruvu katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na Coastal itamenyana na Ecofoot katika mechi ya kusaka bingwa mpya wa michuano hiyo keshokutwa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YATINGA FAINALI BURUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top