• HABARI MPYA

    Saturday, July 14, 2012

    NYIGU WAING'ATA NGORONGORO 2-0


    Michelsen, kocha wa Ngorongoro

    Na Prince Akbar
    TIMU ya taifa ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, leo imefungwa 2-0 na Rwanda kwenye Uwanja wa Chamazi, katika mchezo wa kirafiki, kujiandaa na mechi dhidi ya Nigeria Julai 29, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika.
    Rwanda ‘Nyigu Wadogo’, waliowasili Dar es Salaam jana mchana Dar es Salaam kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ngorongoro Heroes, leo waliizidi uwezo Ngorongoro.
    Rwanda yenye msafara wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20, ambayo imefikia katika hoteli ya Sapphire, baada ushindi huo wa leo, itarudiana na Ngorongoro keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ngorongoro Heroes iko kambini chini ya Kocha wake, Mdenmark Jakob Michelsen na msaidizi wake Mohamed Adolf Rishard.
    Mechi dhidi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NYIGU WAING'ATA NGORONGORO 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top