 |
| Atletico wakishangilia bao la pili |
MABAO mawili ya Olivier Ndikumana katika dakika ya 81 na
90+3, jioni hii yameipa Atletico FC ushindi wa 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi,
Yanga katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga leo ilicheza ovyo na ilizidiwa katika kila idara-
angalau baada ya kufungwa bao la kwanza walijaribu kushambulia kwa mipira ya
pembeni, lakini walipopigwa la pili katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza
baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo ‘walitepeta kabisa’.
Katika mechi ya kwanza ya kundi hilo, APR ya Rwanda
iliitandika 7-0 Waw Salam ya Sudan Kusini.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Yanga, Tom Saintfiet alisema kwamba Atletico ni timu nzuri na na walicheza vizuri, lakini timu yake haikuwa vizuri leo. Aidha, alisema alipokuja Yanga aliambiwa timu hiyo inacheza mpira wa kukimbiza, ambao yeye hakuutaka.
"Nataka wacheze soka ya utulivu, lakini leo mambo hayakuwa mazuri, taratibu timu itaendelea kuimarika na bado nina matumaini ya kufanya vizuri,"alisema.
Lakini kocha wa Atletico, Kaze Cedric aliiponda safu ya ulinzi ya Yanga, kwamba ilikuwa butu. "Niliiogopa Yanga, nilijua ina wachezaji wazuri, tulijua tutapata upinzani mkubwa, lakini nashukuru tumeshinda. Tulijua Yanga wana kasi, tukaanza kwa kuwatuliza,"alisema Kaze.
 |
| Refa wa mechi ya leo, Dennis Batte wa Uganda |
 |
| Huyu kipa aliyedaka leo Atletico, anaitwa Kaseja kwa jina la utani, ila jina lake halisi ni Said Ndikumana |
 |
| Kampeni zinaendelea |
 |
| Yanga kama wamemwagiwa maji, kufungwa noma |
 |
| Mtakatifu Tom akimpa 'bravo' kocha wa Atletico, Kaze |
 |
| Yanga wapolee |
 |
| Muuwaji wa Yanga, Olivier Ndikumana alivaa jezi namba 7 |
 |
| Hatari kwenye lango la Atletico |
0 comments:
Post a Comment