Andy Carroll; sasa ataenda Fulham?


Tetesi za Ijumaa magazeti ya Ulaya

JOEY BARTON ATOLEWA KWA MKOPO DARAJA LA KWANZA HUKO 

KLABU ya Queens Park Rangers inataka kumtoa kwa mkopo kiungo mtukutu, Joey Barton, mwenye umri wa miaka 29, kwenda klabu ya Daraja la Kwanza, na Blackburn ndio inaongoza mbio za kumnasa mchezaji huyo.
KLABU ya Fulham inatumai pauni Milioni 9 pamoja na Clint Dempsey, mwenye umri wa miaka 29, zitatosha kwa Liverpool kumruhusu mshambuliaji Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, ahamie Craven Cottage.
Nathaniel Clyne
Nathaniel Clyne alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Crystal Palace 2011
KLABU ya Liverpool imekubali dili la pauni Milioni 12 kumnasa Fabio Borini, mwenye umri wa miaka 21, awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha wao mpya, Brendan Rodgers, na Mtaliano huyo anatarajiwa kukamilisha usajili wake mwishoni mwa wiki.
KUSAJILIWA kwa Fabio Borini kutahitimisha zama za Craig Bellamy katika Uwanja wa Anfield, na QPR na Cardiff zote zinaiwania saini ya mshambuliaji huyo wa Liverpool.
KLABU ya Tottenham inaelekea kuwapiga bao Arsenal katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Adrian Lopez, mwenye umri wa miaka 24, na wako tayari kutoa dau la pauni Milioni 15 kumaliza suala lake.
KOCHA wa Porto, Vitor Pereira amesema kwamba Tottenham inamtaka Joao Moutinho, mwenye umri wa miaka 25, lakini amesistiza klabu hiyo ya White Hart Lane itatakiwa kulipa pauni Milioni 31.5 kumnasa kiungo huyo.
BEKI wa Manchester City, Kolo Toure, mwenye umri wa miaka 31, anatakiwa na Bursaspor, na klabu hiyo ya Uturuki iko tayari kulipa pauni Milioni 6, kwa mchezaji huyo ambaye alisajiliwa kwa dau la pauni Milioni 16 mwaka 2009.
KLABU ya Southampton inatumai kumnasa beki wa kulia wa Crystal Palace, Nathaniel Clyne, mwenye umri wa miaka 21.

FERGUSON KUTUA NOTTNGHAM

MMILIKI mpya wa klabu ya Nottingham Forest, anamtaka kocha wa Peterborough, Darren Ferguson, mwenye umri wa miaka 40, aifundishe timu hiyo baada ya kumfukuza Steve Cotterill.
Peterborough manager Darren Ferguson
Darren Ferguson alichukua kazi Peterborough kwa mara ya pili Januari 2011
MCHEZAJI wa West Ham, Ricardo Vaz Te, mwenye umri wa miaka 25, anatafakari mustakabali wake katika klabu ya West Ham, baada ya kukwama kwa ombi lake la nyongeza ya mshahara.
Kyle Walker, mwenye umri wa miaka 22, amesema kwamba chumba cha kuvalia nguo cha Tottenham kitampa fursa ya mafanikio kocha mpya wa klabu hiyo, Andre Villas-Boas katika Uwanja wa White Hart Lane. "Anaenda kutupa nafasi, nasi tunaenda kumpa nafasi. Matumaini ni kufanhya vema na kutwaa mataji."