• HABARI MPYA

    Wednesday, June 17, 2026

    AUSTRIA YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA YAICHAPA JORDAN 3-1


    TIMU ya Austria imeibuka ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jordan katika mchezo wa Kundi J Fainali za Kombe la Dunia Asubuhi ya leo Uwanja wa Levi's, Santa Clara, California, Marekani.
    Mabao ya Austria yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Werder Bremen ya Ujerumani, Romano Christian Schmid dakika ya 21, beki wa kati wa FC Seoul ya Korea Kusini, Yazan Mousa Mahmoud Abu Al-Arab aliyejifunga dakika ya 77 na mshambuliaji wa Red Star Belgrade ya Serbia, Marko Arnautović dakika ya 90’+12 kwa penalti.
    Bao pekee la Jordan na la kufutia machozi katika mchezo huo uliochezeshwa na refa maarufu wa Afrika, Dahane Beida wa Mauritania limefungwa na mshambuliaji wa Al-Sailiya ya Qatar, Ali Iyad Ali Olwan dakika ya 50.
    Ikumbukwe mchezo wa kwanza wa Kundi hilo - mabingwa watetezi, Argentina waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Algeria Uwanja wa Arrowhead, Kansas City, Missouri, Marekani. 
    Mabao yote ya Argentina yamefungwa na mshambuliaji wa Inter Miami ya Marekani, Lionel Andrés Messi dakika ya 17, 60 na 76 ambaye Juni 24 mwaka huu atatimiza miaka 39 tangu azaliwe huko Rosario, Santa Fe na hiyo ikiwa hat-trick ya kwanza kwenye michuano hiyo aliyoanza kucheza mwaka 2006 nchini Ujerumani
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AUSTRIA YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA YAICHAPA JORDAN 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top