// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RONALDO FITI ASILIMIA 100 KWA FAINALI LIGI YA MABINGWA, ATAPANGWA LEO MECHI YA MWISHO LA LIGA KUPASHA KWANZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RONALDO FITI ASILIMIA 100 KWA FAINALI LIGI YA MABINGWA, ATAPANGWA LEO MECHI YA MWISHO LA LIGA KUPASHA KWANZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, May 17, 2014

    RONALDO FITI ASILIMIA 100 KWA FAINALI LIGI YA MABINGWA, ATAPANGWA LEO MECHI YA MWISHO LA LIGA KUPASHA KWANZA

    KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kwamba Cristiano Ronaldo amepona tena baada ya kuumia maumivu ya nyama katika mchezo dhidi ya Valladolid.
    Mreno huyo alilazimika kutoka nje Madrid ikilazimishwa safe ya 1-1 katika mechi ya La Liga na akakosa mchezoa ambao timu yake hiyo ilifungwa 2-0 na Celta Vigo mwishoni mwa wiki iliyopita.
    Lakini akizungumza kuelekea mchezo wa leo na Espanyol, Ancelotti alisema kwamba nyota wake huyo atacheza katika sehemu fulani ya mchezo huo wa mwisho wa msimu wa nyumbani.

    Maneno ya busara: Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kulia) akimsikiliza mocha Carlo Ancelotti (wa taut kutoka kulia) katika mazoezi ya jana

    Alipoulizwa kama Ronaldo amepona maumivu yake, mocha huyo wa zamani wa Chelsea alisema: "Cristiano yuko vizuri na atacheza kesho (leo),".
    Habari zitakuwa ahueni kubwa kwa mashabiki wa Los Blancos, ambao tayari wanautazama mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi ijayo dhidi ya wapinzani wao wa nyumbaniu, Atletico Madrid baada ya kutupwa nje ya mbio za ubingwa wa Hispania.
    Xabi Alonso ataukosa mchezo wa Lisbon baada ya kupewa kadi ya nano katika Nusu Fainali Real wakiifunga Bayern Munich, lakini Ancelotti anafurahishwa na viungo wa kati waliopo.
    Amesema: "(Asier) Illarramendi ni suluhisho la kwanza, kwa sababu tulimsajili kuchukua nafasi ya Xabi (Alonso) na anajua namna ya kucheza katika nafasi hii. Illarra ana ubora wa kutosha kucheza katika mechi zote, muhimu ni kwamba tunafurahi kuwa naye,".
    Preparation: Real players have a Champions League final with rivals Atletico Madrid to look forward to
    Maandalizi: Wachezaji wa Real wanakabiliwa na fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya mahasimu wao wa nyumbani, Atletico Madrid

    Sami Khedira yuko pia kwenye nafasi ya kuziba pebgo la Alonso baada ya kupona maumivu yake ya muds mrefu ya goto na Ancelotti amesema kwamba Mjerumani huyo atacheza dhidi ya Espanyol.
    "Khedira atapewa dakika kadhaa kesho (leo) kwa sababu anahitaji kucheza. Alkifanya vizuri dhidi ya Celta Vigo,"alisema. "Anaweza kuwa sukuhisho kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO FITI ASILIMIA 100 KWA FAINALI LIGI YA MABINGWA, ATAPANGWA LEO MECHI YA MWISHO LA LIGA KUPASHA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top