// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); REAL MADRID YAMALIZA KWA HESHIMA LA LIGA BILA RONALDO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE REAL MADRID YAMALIZA KWA HESHIMA LA LIGA BILA RONALDO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, May 17, 2014

    REAL MADRID YAMALIZA KWA HESHIMA LA LIGA BILA RONALDO

    REAL Madrid imemaliza kwa heshima msimu wa La Liga baada ya kuifunga mabao 3-1 Espanyol Uwanja wa Santiago Bernabeu jioni hii.
    Ushindi huo unaifanya Real imalize msimu huu wa La Liga na pointi 87 baada ya kucheza mechi zote 38 na inaweza ikawa ya pili ya tatu baada ya mechi zote, itategemea na matokeo ya mchezo kati ya Barcelona na Atletico Madrid unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Camp Nou.  
    Bado gonjwa; Cristiano Ronaldo ameendelea kuwa nje kwa maumivu ya nyama 

    Mabao ya Real yalifungwa na Gareth Bale dakika ya 64 akimalizia pasi ya Karim Benzema, Alvaro Morata mawili dakika ya 86 na 90, wakati bao pekee la Espanyol lilifungwa na Pizzi dakika ya 90 pia.
    Real ilendelea kumkosa mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo anayesumbuliwa na maumivu ya nyama, ambaye awali iliripotiwa angecheza sehemu ya mchezo wa leo. Hi-five: Gareth Bale (right),celebrating with Angel Di Maria put Real ahead in their 3-1 win over Espanyol
    Kula tano: Gareth Bale (kulia), akishangilia na Angel Di Maria baada ya kuifungia Real katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Espanyol
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REAL MADRID YAMALIZA KWA HESHIMA LA LIGA BILA RONALDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top