KLABU ya Manchester United imepanga kumvaa kichwa kichwa beki wa Arsenal, Bacary Sagna wiki ijayo kuwania saini yake.
BIN ZUBEIRY inafahamu mabosi wa Old Trafford kwa takriban saa 48 sasa wamekuwa wakiwasaka wawakilishi wa beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Kama tulivyoandika awali Sagna atakuwa na mazungumzo na wawakilishi wa Manchester City wiki ijayo kwa ajili ya kujadili mkataba wa miaka minne, utakaomfanya alipwe mshahara wa si chini ya Pauni 100,000 kwa wiki.
Anagombewa: Manchester United na City zone zinataka kumsaini beki wa Arsenal, Bacary Sagna kwa ajili ya msimu ujao
Klabu hiyo ya Either imepiga hatua zaidi katika kuwania saini ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa- lakini United inataka kuwapiga bao wapinzani wao wa Jiji kwa kumsajili mchezaji huyo.
Kocha ajaye United, Louis van Gaal amemuelezea Sagna kama mtu anayemuhitaji akashirikiane na Rafael katika beki ya kulia.



.png)
0 comments:
Post a Comment