Na Ilham Khalid, Dar es Salaam
GEOGRE Wakuganda ni mmoja wa wagombea waliojitokeza kuwania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba inayotarajia kufanya uchaguzi Juni 29 mwaka huu.
Wakuganda anawania nafasi hiyo akiwa na wajumbe wenzake 32 waliojitokeza kuchukua fomu na kurudisha kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Wakuganda alisema kuwa anajiamini ana uwezo wa kuiongoza Simba kwa kuwa ana weledi mkubwa.
“Wana Simba wanajua uwezo wangu na naamini uwezo ninao nguvu ninazo wanachotakiwa ni kuirudisha Simba katika hadhi yake,”alisema
Wakuganda alisema kuwa moja ya sababu zilizomfanya achukue fomu ni kutaka mchango wake sambamba na kuondoa migogoro na mpasuko kwenye klabu hiyo.
"Naamini nina uwezo na Wanasimba wanatambua uwezo wangu, nilianza kuitumikia Simba tangu nikiwa mdogo, hivyo wananielewa kazi zangu,”alisema
Alieleza kwamba huu ni wakati wa Simba kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua viongozi watakaoisaidia klabu yao katika miaka minne ijayo.
"Naomba nisiseme sana kwa sababu muda wa kampeni na kutangaza sera zetu haujafika", alisema mgombea huyo.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Simba, Damas Ndumbalo leo anatarajia kuanika majina ya wagombea wanaowania nafasi ya uongozi kwenye timu hiyo.
Alisema wanachama 41 kutoka sehemu mbalimbali nchini walichukua fomu na kurudisha kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo inayotarajia kufanya uchaguzi mkuu Juni 29 mwaka huu.

![]() |
George Wakuganda anataka Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Simba SC |

0 comments:
Post a Comment