• HABARI MPYA

    Tuesday, January 15, 2013

    WAMBURA AJITOSA TFF UMAKAMU WA RAIS, BALHABOU NAYE NDANI

    Michael Wambura

    Na Boniface Wambura
    IDADI ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.
    Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
    Waliochukua leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.
    Idadi kamili ya waliochukua ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
    Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
    Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
    Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
    Wakati huo huo: Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Soka Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
    Mkoa utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WAMBURA AJITOSA TFF UMAKAMU WA RAIS, BALHABOU NAYE NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top