• HABARI MPYA

    Tuesday, January 15, 2013

    AZAM WAENDA KENYA KUCHEZA MECHI TATU ZA MAANA

    Azam na Kombe la Mapinduzi

    Na Mahmoud Zubeiry
    BAADA ya kutwaa Kombe la Mapinduzi mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar, Azam FC inatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya wiki moja ya michezo ya kirafiki, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.
    Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba katika ziara hiyo watacheza mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya timu za Sofapaka, AFC Leopards na Gor Mahia kabla ya kurejea nchini Januari 23.
    Nassor alisema ziara hiyo ni maalum kwa ajili ya kuiweka sawa timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
    Nassor amesema anaamini timu za Kenya ni nzuri na zitawapa changamoto nzuri kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na kuingia kwenye Kombe la Shirikisho.
    “Tumekuwa katika programu ndefu ya maandalizi tangu Desemba, tukianzia Kongo (DRC) ambako tulicheza mashindano na kuchukua Kombe, tumetoka tumeingia kwenye Kombe la Mapinduzi tumeshiriki na kuchukua Kombe, na sasa tunakwenda Kenya,”alisema Nassor.
    Katibu huyo alisema kikosi kizima cha Azam kitakwenda Kenya kwenye ziara hiyo na baada ya hapo timu itarejea tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM WAENDA KENYA KUCHEZA MECHI TATU ZA MAANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top