• HABARI MPYA

    Sunday, September 16, 2012

    SIMBA WAONGOZA KWA MAPATO MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU

    Nassor Masoud 'Chollo' wa Simba akitia krosi katika mechi ya jana

    Na Prince Akbar
    MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.
    Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
    Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
    Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
    Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.
    Aidha, watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
    Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
    Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAONGOZA KWA MAPATO MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top