• HABARI MPYA

    Monday, September 24, 2012

    YANGA YAPOTEZA POINTI ZA JKT KWA KUCHEZESHA WAGENI WATANO

    Kikosi cha Yanga kilichomenyana na JKT, kutoka kulia waliosimama Berko, Yondan, Chuji, Kavumbangu, Joshua,  na Cannavaro. Waliopiga magoti kutoka kulia ni Twite, Kiiza, Msuva, Niyonzima na Nizar.

    Na Mahmoud Zubeiry
    YANGA iko hatarini kupokonywa pointi tatu ilizovuna kutokana na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kuzidisha idadi ya wachezaji wa kigeni.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Wallace Karia ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji watano wa kigeni, lakini itaruhusiwa kutumia watatu tu kwa wakati mmoja.
    Alisema mabadiliko ya kanuni za wachezaji wa kigeni, kutoka watano hadi 10 kusajiliwa na watano kucheza kwa wakati mmoja, yataanza kutumika msimu ujao.
    “Tunatarajia kukutana keshokutwa kupitia ripoti za mechi zote, ikiwemo mechi ambayo Emmanuel Okwi alimpiga mchezaji mwenzake ngumi, baada ya kikao tutatoa ripoti ya maamuzi,”alisema Karia.
    Jumamosi, Yanga ikimenyana na JKT Ruvu, Mgahan Yawe Berko, alianza langoni, Wanyarwanda Mbuyu Twite alicheza beki ya kulia, Haruna Niyonzima alicheza kiungo cha juu, Mrundi Didier Kavumbangu na Mganda Hamisi Kiiza walicheza mbele.  
    Kikosi cha Yanga siku hiyo kilikuwa; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte Ally, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon Msuva.
    Uzembe huu, moja kwa moja unatokana na mabadiliko yaliyofanywa Ijumaa, kumuondoka Meneja wa timu, Hafidh Saleh bila kuteua Meneja mpya na pia unadhihirisha ukosefu wa umakini wa benchi la ufundi la sasa, chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Freddy Felix Minziro, anayekaimu nafasi hiyo baada ya kufukuzwa kwa Mbelgiji, Tom Saintfiet.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAPOTEZA POINTI ZA JKT KWA KUCHEZESHA WAGENI WATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top