• HABARI MPYA

    Thursday, September 27, 2012

    MAZOEZI YA SIMBA KWEREKWE YANGA AKIPONA MUNGU WAO


    Na Mahmoud Zubeiry
    SIMBA SC inaendelea vizuri na maandalizi yake ya pambano dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 3, mwaka huu, ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Kiislam, Kwerekwe, visiwani Zanzibar na kambi yao ipo Chukwani.
    Morali ya kambi ipo juu na wachezaji wote wako fiti, wakijifua kwa shauku kubwa ili kumvutia kocha Mserbia, Milovan Cirkovick awape nafasi ya kucheza Oktoba 3, kuanzia sa 1:00 usiku.
    Simba itarejea Dar es Salaam Jumamosi kucheza mechi na Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, kisha kurejea tena visiwani humo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa Jumamosi ijayo.
    Hata hivyo, katika michezo miwili ijayo, Simba itamkosa mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi ambaye amefungiwa na Kamati ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya Mwenyekiti wake, Wallace Karia kufuatia kikao cha juzi, sambamba kumtoza faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu, Kessy Mapande.
    Okwi alifanya hivyo akilipa kisasi cha kuchezewa rafu Jumatano iliyopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Tayari Okwi amekosa mechi moja ya juzi dhidi ya Ruvu Shooting na wakati, na sasa atakosa mechi mbili zaidi, dhidi ya Prisons na dhidi ya Yanga na baada ya hapo atakuwa huru kuendelea kumtukia mwajiri wake.
    Siyo siri, kuelekea pambano la watani wa jadi, Okwi alikuwa ni homa kwa Yanga, hasa wakikumbuka namna alivyowanyanyasa katika mechi iliyopita, akifunga mabao mawili kwenye ushindi wa 5-0 na kusababisha mawili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZOEZI YA SIMBA KWEREKWE YANGA AKIPONA MUNGU WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top