Saintfiet akipanda basi jipya la Yanga baada ya kumaliza kuzungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Jangwani. |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA Mkuu
wa Yanga SC, Mbelgiji Tom Saintefiet ameteua wachezaji 18 kwa ajili ya mchezo
wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya JKT Ruvu, kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, safari hii akimchukua mshambuliaji Jerry Tegete na
kumtema Said Bahanuzi.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga
na Jangwani, Dar es Salaam, Mbelgiji huyo alisema anaelekea kukatishwa tamaa na
wachezaji wake hivi sasa juu ya viwango vyao.
Alisema hata
kufunga penalti, hivi sasa imekuwa ni tatizo na mazoezini jana akiwajaribu kwa penalti
wachezaji wake, kati ya mastaa wake sita, waliofunga ni wawili tu. “Yaani hata kesho
siombei nipate penalti, maana sijui kama tutaweza kuitumia vizuri,”alisema
Mtakatifu Tom.
Aliwataja wachezaji
aliowateua kwa ajili ya mechi ya kesho, ambayo itakuwa ya tatu tangu kuanza kwa
Ligi Kuu ni makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul,
Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin Yondan,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano
Mwasyika.
Aliwataja
viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Rashid Gumbo,
Shamte Ally na Simon Msuva, wakati washambuliaji ni Jerry Tegete, Didier
Kavumbangu na Hamisi Kiiza na ambao hawamo kwenye programu ya kesho ni kipa
Said Mohamed, mabeki Nsajigwa Shadrack, Job Ibrahim, viungo Frank Domayo, Juma
Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin Bakari, Idrisa Assega, na Issa
Ngao wa Yanga B anayekomazwa kikosi cha kwanza na mshambuliaji Said Bahanuzi.
Yanga imeambulia
pointi moja tu katika mechi zake mbili za Ligi Kuu, awali ikilazimishwa sare ya
bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na
Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Huo ulikuwa
mchezo wa pili Saintfiet anafungwa Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo
tangu ajiunge nayo, Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin
Bozidar Papic.
Katika mechi
hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico
ya Burundi.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga
Vs JKT Ruvu (Kirafiki) 2-0
2.
Yanga
Vs Atletico (Burundi, Kagame) 0-2
3.
Yanga
Vs Waw Salam (Sudan, Kagame) 7-1
4.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 2-0
5.
Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame) 1-1 (5-3penalti)
6.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 1-0
7.
Yanga
Vs Azam (Kagame) 2-0
8.
Yanga
Vs African Lyon (Kirafiki) 4-0
9.
Yanga
Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda) 2-0
10.
Yanga
Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda) 2-1
11.
Yanga
Vs Coastal Union (Kirafiki) 2-1
12.
Yanga
Vs Moro United (Kirafiki) 4-0
13.
Yanga
Vs Prisons (Ligi Kuu) 0-0
14.
Yanga
Vs Mtibwa (Ligi Kuu) 0-3
0 comments:
Post a Comment