• HABARI MPYA

    Sunday, July 15, 2012

    HAYE AMCHAPA KO RAUNDI YA TANO CHISORA


    David Haye akimtupia kitu Chisora katika Uwanja wa Upton Park usiku wa kuamkia leo
    AMEKOMA! Kama ingekuwa bongo ndivyo ambavyo Dereck Chisora angeimbiwa baada ya kutandikwa na bingwa wa zamani wa WBO na WBA uzito wa juu, David Haye, kwa Knockout (KO) ya raundi ya tano katika pambano la ngumi la uzito wa juu lililofanyika ujsiku wa kuamkia leo Uwanja wa Upton  Park.
    Haye alikutana na kibonde haswa ulingoni, kwani alitawala pambano hilo tangu mwanzo, tena akipigana kwa kujiamini, dhidi ya Chisora ambaye alipiga ngumi ya kwanza ya kwenye uso wa Haye katika raundi ya tatu.
    Chisora ambaye alitamba ataingia katika pambano hilo kama kichaa na kuahidi kumuangusha Haye raundi ya saba, alijikuta akidondoshwa chini mara mbili katika raundi ya tano kama gunia la nafaka na pambano likaishia hapo.
    Alitandikwa ngumi mbili, ya kulia na ya kushoto upande wa chini ya shavu la kushoto na kulia, akachanganyikiwa na kuifuata sakafu kwa mara ya kwanza mapema katika raundi ya tano, ingawa aliinuka baada ya kuhesabiwa na kuendelea na pambano.
    Sekunde chache tu baada ya kurudi mchezoni, Haye alimsogelea haraka Chisora na kuanza tena kumtandika ngumi mfululizo- alimpiga ngumi tano mfululizo zilizoingia sawia kwenye taya na usoni, hivyo kumpeleka chini kwa mara nyingine na huo ndio ukawa mwisho wa pambano.
    Ushindi huo unamfanya Haye mwenye urefu wa futi 6 na inchi 3 sasa awe ameshinda mapambano 26 (24 kwa KO) na amepigwa mawili wakati hajatoka sare, na Chisora amefikisha mapambano manne ya kupigwa, kushinda 15 (9 kwa KO) na hajatoka sare.
    Hilo lilikuwa pambano la kwanza kwa Haye, tangu alitangaza kustaafu ndondi, baada ya kuchapwa na Vladimir Klitschko Julai 2011 na kupoteza taji lake la WBA.


    Anaenda chini: Chisora akdondoka chini baada ya kuchapwa na from Haye


    Amekoma: Chisora anahesabiwa na refa Luis Pabon

    Chali: Haye akisogea pembeni baada ya kumbwaga chini Chisora

    Machungu ya kipigo: Chisora akilalamika baada ya kupigwa kwa Knockout (KO) na Haye

    Mwanzo kabisa: Haye na Chisora wakipewa maelekezo kabla ya pambano.

    Nyomi: Umati wa watu ulioshuhudiwa pambano hilo.
    SOURCE: http://www.dailymail.co.uk

     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAYE AMCHAPA KO RAUNDI YA TANO CHISORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top