• HABARI MPYA

    Friday, July 08, 2016

    MOURINHO ATHIBITISHIWA WASAIDIZI MAN UNITED, NI WALE WALE WA SIKU ZOTE

    WASAIDIZI wa kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho wamethibitishwa.
    Msaidizi namba moja mwaminifu wa Mourinho, Rui Faria amekuwa Kocha Msaidizi wa Mashetani hao Wekundu. 
    Mourinho alikutana kwa mara ya kwanza Faria Barcelona kabla ya kufanya naye kazi klabu ya Uniao de Leiria ya Ureno kama kocha wa mazoezi ya viungo na akaenda naye Chelsea mara zote mbili, Inter Milan na Real Madrid.
    Kocha Silvino Louro, ambaye amekuwa na Mourinho kwa zaidi ya muongo mmoja kama kocha wake wa makipa, pia ametajwa katika jopo la makocha wanne wasaidizi wa Mreno huyo Old Trafford.
    Jose Mourinho akiwa na Faria (kushoto) na Steve Holland wakati wakifundisha Chelsea  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    Ricardo Formosinho na Carlos Lalin - ambao pia wana uzoefu wa kufanya kazi na Mreno huyo awali - na Emilio Alvarez pia wamethibitishwa katika benchi la Ufundi pamoja na mtathmini, Giovanni Cerra. 
    Uthibitisho wa United wa benchi hilo la Ufundi unakuja baada ya Mourinho kujivua lawama za kuondoka kwa Ryan Giggs aliyekuwa Kocha Msaidizi namba moja kwamba hahusiki.
    Katika mkutano wa kumtambulisha rasmi Jumanne Old Trafford, Mourinho alisema kwamba ilikuwa ni vigumu kwa winga huyo wa zamani wa United kubaki kulingana na mazingira.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOURINHO ATHIBITISHIWA WASAIDIZI MAN UNITED, NI WALE WALE WA SIKU ZOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top