• HABARI MPYA

    Friday, July 15, 2016

    MALINZI AWAPONGEZA WANAMICHEZO WALIOPEWA MAJUKUMU NA RAIS MAGUFULI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi, Francis Ndulane.
    Kuuli, Wakili msomi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF, ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga mkoani Tabora.
    Kadhalika, katika uteuzi huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Ndulane ambaye ni Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro.
    Katika salamu hizo, Rais Malinzi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwateua viongozi hao wa TFF, akisema kwamba ameonyesha namna alivyo na imani na watendaji hao katika shughuli zao mbalimbali ikiwamo TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AWAPONGEZA WANAMICHEZO WALIOPEWA MAJUKUMU NA RAIS MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top