TIMU ya Middlesbrough iliyorejea Ligi Kuu ya England imeendelea na pilika za usajili baada ya kufanikiwa kuipata saini ya beki wa Valencia, Antonio Barragan kwa mkataba wa mika mitatu.
Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 29, ambaye aliwahi kuchezea Liverpool alipokuwa anachipukia, anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na timu hiyo ya Kaskazini Mashariki katika harakati za kocha Aitor Karanka kukiongezea nguvu kikosi chake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Middlesbrough imemsajili beki wa kulia wa Valencia, Antonio Barragan kwa Mkataba wa miaka mitatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Barragan anaungana na Victor Valdes, Viktor Fischer, Bernardo Espinosa, Marten de Roon na Jordan McGhee kwenye kikosi cha Karanka na Boro inatumai mchezaji mwenzake wa zamani wa Valencia, Alvaro Negredo anaweza kumfuata kutokana na juhudi zinaozendelea hivi sasa za kutaka kumsajili.Barragan aliondoka Liverpool mwaka 2006 na amechezea Deportivo na Real Valladolid kabla ya kujiunga na Los Che, ambako alipata nafasi nzuri ya kuonyesha uwezo wake.
0 comments:
Post a Comment