• HABARI MPYA

    Thursday, September 13, 2012

    KAPOMBE KUONGEZEWA MSHAHARA SIMBA, SASA KULIPWA SAWA NA KASEJA, KAZIMOTO

    Kapombe kulia akiwa amebeba Ngao aliitolea jasho la kutosha tu juzi, Kushoto ni Meneja Vifaa vya michezo wa Simba, Kessy Kaburu

    Na Mahmoud Zubeiry
    KIRAKA Shomary Kapombe anapigiwa debe aongezewe mshahara kutoka Sh, 800,000 anazolipwa sasa hadi Sh, Milioni 1, sawa na mastaa wengine wa Simba, mfano Juma Kaseja na Mwinyi Kazimoto, ambao wote hawafui dafu kwa Mrisho Ngassa anayelipwa Sh. Milioni 2.
    Habari kutoka ndani ya Simba, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zinasema kwamba, Kapombe aliongezewa mshahara kutoka Sh. 400,000 baada ya beki Kevin Yondan kutimkia Yanga na miezi mitatu badaaye, yuko kwenye nafasi ya kuongezewa 200,000 zaidi.
    Hata akipewa Milioni 1, bado Kapombe hatawafikia mabeki wa kigeni Komabil Keita na Paschal Ochieng ambao bila kupepesa macho, wote hawamfikii kwa uwezo wa kazi uwanjani.
    Kapombe amekuwa akiibeba mno Simba katika mechi za karibuni na ushindi wa Ngao ya Jamii juzi, mabao 3-2 dhidi ya Azam FC, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar e s Salaam mchezaji huyo alifanya kazi kubwa mno.
    Kapombe anaweza kucheza beki ya kulia, beki wa kati na nafasi yoyote ya kiungo kuanzia ukabaji, pembeni na katikati.
    Siyo tu soka anaijua, bali pia Kapombe hujituma uwanjani, ingawa siku zote ukikutana naye nje ya Uwanja ni kijana mpole na mtiifu. Kapombe si tegemeo kwa Simba SC tu, bali hata timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
    Huwezi amini, Mwanamichezo huyo bora wa TASWA ndio kwanza anaingia katika msimu wake wa pili Simba SC tangu asajiliwe kutoka Polisi Morogoro, wakati huo ikiwa Daraja la Kwanza. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAPOMBE KUONGEZEWA MSHAHARA SIMBA, SASA KULIPWA SAWA NA KASEJA, KAZIMOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top