• HABARI MPYA

    Tuesday, July 10, 2012

    WAPINZANI WA YANGA WA KWANZA KUWASILI DAR KOMBE LA KAGAME


    Atletico FC itakayofungua dimba na Yanga

    Na Princess Asia
    KLABU za El Salam Wau ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi zinatarajiwa kuwa timu za kwanza kuwasili nchini kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
    Michuano hiyo inaanza kutimua vumbi Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikishirikisha timu kumi na moja akiwemo bingwa mtetezi Yanga na makamu bingwa Simba.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY mchana wa leo kwamba, kikosi cha El Salam Wau ambacho kitawasili kesho alfajiri (Julai 11 mwaka huu) kwa ndege ya Ethiopia Airlines kikitokea Juba kupitia Addis Ababa, Ethiopia kikiwa na wachezaji 18 na viongozi saba.
    Amewataja wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Khamis Leone Uso Wani (nahodha), Adheil Bugwic Jongkor Bugwic, Edward Joram Simon Julio, Fidel Andrea Fides Fas, Ismael Musa Juma Ismael, James Anei Matheli Anei, Jervas Ayo Abdalla Ayak, Khamis Doshama Ulama Andel na Meki Sultan Berema Kuku.
    Amewataja wengine ni Moga Emmanuel Androga, Mubarak Mohammed Saleh Omer, Ndili Rabeh Nasir Hozi, Nizir Rihan Taban Talib, Oliver Paul Kangi Akok, Rabie Mohammed Abubakar Hassan, Rufino Joseph Uras Ambros, Santino Makuei Uyu Upio, Thomas Rufino Thomas Diakon.
    Amesema Atletico nao wanatarajiwa kuwasili kesho (Julai 11 mwaka huu) kwa usafiri wa barabara. Timu hiyo inakuja kwa usafiri wa basi lake ambalo pia italitumia kwa muda wote itakapokuwa kwenye mashindano.
    Amesema wakati El Salam Wau itafikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo, Atletico itakuwa Lunch Time Hotel iliyoko Mabibo.
    Amezitaja timu zinazotarajiwa kuwasili keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) ni Mafunzo ya Zanzibar kwa boti saa 9 alasiri, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) itatua saa 1.20 usiku kwa Kenya Airways. Timu nyingine itakayowasili siku hiyo jioni ni URA ya Uganda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAPINZANI WA YANGA WA KWANZA KUWASILI DAR KOMBE LA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top