• HABARI MPYA

    Wednesday, July 11, 2012

    MAREFA WA KAGAME WAPIMWA UTIMAMU WA MWILI


    Na Prince Akbar
    MTIHANI wa utimamu wa mwili (fitness test) kwa waamuzi walioteuliwa kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame inayoanza Jumamosi (Julai 14 mwaka huu) utafanyika kesho (Julai 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, waamuzi 15 walioteuliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuchezesha michuano hiyo. Waamuzi hao wanawasili leo jijini Dar es Salaam.
    Wambura amesema kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
    Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA WA KAGAME WAPIMWA UTIMAMU WA MWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top