• HABARI MPYA

    Thursday, May 21, 2026

    NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE KWA MBEYA CITY, 1-1 UWANJA WA MAJALIWA


    WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
    Winga Hassan Salum Kabunda alianza kuifungia Namungo FC dakika ya sita, kabla ya mshambuliaji Eliud David Ambokile kuisawazishia Mbeya City dakika ya 28.
    Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 25 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 12, wakati Mbeya City inafikisha pointi 22,  ingawa inabaki nafasi ya 14 baada ya timu hizo zote kucheza mechi 24 kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. 
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja, wakati nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.   

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE KWA MBEYA CITY, 1-1 UWANJA WA MAJALIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top