• HABARI MPYA

  Friday, July 15, 2016

  BORO YASAINI WA SITA, NI BEKI LA LA LIGA LILILOWAHI KUKIPIGA LIVERPOOL

  TIMU ya Middlesbrough iliyorejea Ligi Kuu ya England imeendelea na pilika za usajili baada ya kufanikiwa kuipata saini ya beki wa Valencia, Antonio Barragan kwa mkataba wa mika mitatu.
  Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 29, ambaye aliwahi kuchezea Liverpool alipokuwa anachipukia, anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na timu hiyo ya Kaskazini Mashariki katika harakati za kocha Aitor Karanka kukiongezea nguvu kikosi chake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.

  Middlesbrough imemsajili beki wa kulia wa Valencia, Antonio Barragan kwa Mkataba wa miaka mitatu  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  WASIFU WA BARRAGAN

  2005-06: Liverpool - Mechi 1 hakufunga bao 0
  2006-09: Deportivo - Mechi 34 mabao 2
  2009-11: Real Valladolid - Mechi 47 bao 1
  2011-16: Valencia - Mechi 140 mabao 2
  Barragan anaungana na Victor Valdes, Viktor Fischer, Bernardo Espinosa, Marten de Roon na Jordan McGhee kwenye kikosi cha Karanka na Boro inatumai mchezaji mwenzake wa zamani wa Valencia, Alvaro Negredo anaweza kumfuata kutokana na juhudi zinaozendelea hivi sasa za kutaka kumsajili.Barragan aliondoka Liverpool mwaka 2006 na amechezea Deportivo na Real Valladolid kabla ya kujiunga na Los Che, ambako alipata nafasi nzuri ya kuonyesha uwezo wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORO YASAINI WA SITA, NI BEKI LA LA LIGA LILILOWAHI KUKIPIGA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top