TIMU ya Tabora United imezinduka na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabao ya Tabora United leo yamefungwa na winga Offen Francis Chikola dakika ya 32 na mshambuliaji Mkongo, Heritier Ma Olongi Makambo dakika ya 52, baada ya kiungo Jacob Raymond Massawe kuanza kuifungia Namungo FC dakika ya nne.
Kwa ushindi huo, Tabora United wanafikisha pointi 28, ingawa wanabaki nafasi ya tano, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 17 nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 17.
0 comments:
Post a Comment