TIMU ya Simba SC imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babata mkoani Manyara.
Mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida alianza kuifungia Simba SC dakika ya 57, kabla ya kiungo Ladack Juma Chasambi kujifunga dakika ya 75 kuipatia bao la kusawazisha Fountain Gate.
Fountain Gate walimaliza pungufu baada ya kipa Mnigeria, John Noble kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90'+3 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 44 na inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 17, wakati Fountain Gate inafikisha pointi 21 za mechi 17 pia nafasi ya sita.
0 comments:
Post a Comment