// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MZIZE NA DUBE KILA MMOJA APIGA MBILI YANGA YASHINDA 6-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MZIZE NA DUBE KILA MMOJA APIGA MBILI YANGA YASHINDA 6-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, February 05, 2025

    MZIZE NA DUBE KILA MMOJA APIGA MBILI YANGA YASHINDA 6-1


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Kengold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yamefungwa na washambuliaji, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo mawili, dakika ya pili na 46, Clement Francis Mzize dakika ya sita na 43, viungo, Muivory Coast Pacome Peodoh Zouzoua dakika ya 39 na Mkenya,  Duke Ooga Abuya dakika ya 84.
    Bao pekee la Kengold katika mchezo wa leo limefungwa dakika ya 90’+3 na kiungo mpya, Suleiman Bwenzi aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mbeya Kwanza ya Championship.
    Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 45 katika mchezo wa 17 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ikiwazidi pointi mbili watani, Simba SC ambao pia wana mechi moja mkononi na kesho wanaweza kuurejea uongozi wakiifunga Fountain Gate huko Babati.
    Kengold hali inazidi kuwa mbaya baada ya matokeo ya leo katika mchezo wa 17 wa msimu ikibaki na pointi zake sita tu na inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MZIZE NA DUBE KILA MMOJA APIGA MBILI YANGA YASHINDA 6-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top