// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YABANWA CHAMAZI, SARE 1-1 NA NAMUNGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YABANWA CHAMAZI, SARE 1-1 NA NAMUNGO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, February 27, 2025

    AZAM FC YABANWA CHAMAZI, SARE 1-1 NA NAMUNGO


    WENYEJI, Azam FC wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Namungo FC walianza kupata bao lililofungwa na Khamis Khalifa dakika ya 12, kabla ya Mgambia, Gibrill Sillah kuisawazishia Azam FC dakika ya 43.
    Azam FC wangeweza kuondoka na ushindi kama si nyota wake, Feisal Salum kukosa penalti iliyopanguliwa na kipa, adhabu ambayo ilitolewa baada ya winga Iddy Suleiman ‘Nado’ kuangushwa kwenye boksi.
    Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 45 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya tatu — na Namungo nayo inatimiza pointi 23 katika mchezo wa 22 pia na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 12 kwenye ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi y 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YABANWA CHAMAZI, SARE 1-1 NA NAMUNGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top