• HABARI MPYA

    Thursday, May 01, 2014

    CHELSEA ILIVYOMTIA UNYONGE LUKAKU MBELE YA MARADONA

    MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku ameshuhudia klabu yake, Chelsea ikitolewa katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu, huku kikosi cha Jose Mourinho kikikosa huduma ya mchezaji huyo iliyemtoa kwa mkopo Everton. 
    Lukaku alikaa mbele na Diego Maradona - aliyehudhuria mechi hiyo pamoja na binti yake Dalma - huku The Blues wakichapwa mabao 3-1 na Atletico Madrid na kupoteza nafasi ya kutinga Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Makocha wa Manchester United, Phil Neville na Paul Scholes pia walikuwepo jukwaani Chelsea ikifutwa kwenye michuano licha ya kutangulia kupata bao kupitia kwa Fernando Torres aliyeifunga klabu yake ya zamani.
    Wangeweza wangekuwa nawe: Romelu Lukaku (kushoto) akiangalia Chelsea ikitaabika mbele ya Atletico Madrid
    Watching on: Phil Neville (left) and Paul Scholes were in attendance for Chelsea's clash with Atletico Madrid
    Phil Neville (kushoto) na Paul Scholes walikuwepo pia

    Huku Mashetani Wekundu wakiwa tayari wamepoteza matumaini ya ubingwa na kufuzu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao, haikufahamika kama wawili hao walikuwa hapo kusaka vpaji kwa niaba ya kocha mkuu wa muda, Ryan Giggs.
    Kocha wa England, Roy Hodgson pia alikuwepo na kuna uwezekano alikwenda kumshuhudia Ashley Cole mwenye umri wa miaka 33 kama atamfaa kwenye kikosi chake cha kombe la dunia.
    Keeping an eye on things: England manager Roy Hodgson (centre) also turned up for the match
    Kocha wa England. Roy Hodgson (katikati) alikuwepo pia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA ILIVYOMTIA UNYONGE LUKAKU MBELE YA MARADONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top