• HABARI MPYA

    Friday, May 02, 2014

    BENFICA YAITOA JUVE, KUMENYANA NA SEVILLA FAINALI EUROPA LEAGUE

    LICHA ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja, Benfica ya Ureno imerudi kwenye fainali ya Europa League kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kutoka sare ya 0-0 na Juventus jana hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1. 
    Juventus ilitengeneza nafasi nyingi nzuri, lakini ikashindwa tu kumtungua kipa wa Benfica, Jan Oblak, ambaye aliokoa michomo mingi ya hatari. 
    Licha ya Benfica kumpoteza mchezaji mmoja dakika ya 67 baada ya refa wa England, Mark Clattenburg kumpa kadi ya pili ya njano kiungo Muargentina, Enzo Perez kwa kumchezea rafu Arturo Vidal, kikosi cha Jorge Jesus kilimudu mchezo. Benfica itakutana na Sevilla ambayo jana nayo imeitoa Valencia, zote za Hispania kwa kuifunga mabao 2-0 na kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya awali kufungwa 3-1 katika mchezo wa kwanza.  
    Tumefuzu: Wachezaji wa Benfica wakisherehekea kutinga fainali ya Europa League kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Juventus, kufuatia sare ya bila kufungana jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENFICA YAITOA JUVE, KUMENYANA NA SEVILLA FAINALI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top