Na Mahmoud Zubeiry
ASILIMIA
tano ya mapato yatakayopatikana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community
Shield) kati ya Simba na Azam Jumanne ijayo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, yatakwenda
kwenye Hospitali ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Ofisa wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Boniphace wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kabla ya kukabidhi
fedha hizo, na shirikisho hilo litakutana na uongozi wa Hospitali ya Temeke
kupanga maeneo ambayo fedha hizo zitatumika kwenye hospitali hiyo.
Mechi hiyo
ya uzinduzi rasmi wa msimu wa 2012/2013 itakayoanza saa 10:00 jioni, viingilio vitakuwa
sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya
chungwa, sh. 15,000 kwa viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.
Kihistoria
hiyo itakuwa mechi ya tano ya Ngao ya Jamii kuchezwa nchini na ya pili
kukutanisha timu nje ya wapinzani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga.
Mtibwa
ilicheza na Yanga mwaka 2009, baada ya Simba kugoma na ikashinda mabao 2-1 na
kutwaa Ngao, wakati kabla ya hapo, mwaka 2001, Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa bado
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager,
ilichezwa mechi ya kwanza ya Ngao kihistoria.
Katika mechi
hiyo, Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba na mwaka juzi Yanga iliifunga
tena Simba kwa penali 3-1 kufuatia sare ya 0-0 na mwaka jana, Simba ilitwaa
Ngao ya kwanza katika historia yake, kwa kuifunga Yanga mabao 2-0.
MABINGWA WA
MECHI ZA NGAO YA JAMII:
Mwaka Mshindi Matokeo
2001 Yanga 2-1 Simba
2010 Yanga 0-0 Simba (3-1penalti)
2011 Simba 2-0 Yanga



.png)
0 comments:
Post a Comment