Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya
JUVE SASA WAAMUA KUMTOA WALCOTT ARSENAL, DILI KUKAMILISHWA JANUARI
Vigogo wa Italia, Juventus ni timu nyingine inayoibuka na mipango ya kumsajili winga wa Arsenal, Theo Walcott, mwenye umri wa miaka 23, katika dirisha dogo Januari.
Wakala wa kipa Pepe Reina, mwenye umri wa miaka 30, amekanusha madai kwamba kipa huyo wa Hispania anataka kuondoka Liverpool.
Real Madrid itakuwa radhi kumuuza Cristiano Ronaldo, mwenye umri wa miaka 27, kwa dau la Euro 200 (Pauni Milioni 160.15) kama hawatamaliza tofauti zao na mchezaji huyo zinazoendelea sasa.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce anamfuatilia mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Anthony vanden Borre, mwenye umri wa miaka 24, katika mpango wake wa kusajili wachezaji watatu huru.
Tottenham inataka kumsajili Nahodha wa Urusi na mshambuliaji wa Arsenal, Andrey Arshavin, mwenye umri wa miaka 31, kufuatia mchezaji huyo mambo yake kumuendea komboEmirates.
ARSENAL YAMPA MKATABA MPYA WENGER
Arsenal inamuandalia mkataba mpya kocha Arsene Wenger, kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Gunners, Ivan Gazidis.
Beki wa Queens Park Rangers, Anton Ferdinand yuko tayari kugoma kumpa mkono Ashley Cole kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Chelsea Uwanja wa Loftus Road.
Cesc Fabregas, mwenye umri wa miaka 25, hataondoka Barcelona kwa mkopo Januari, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake, Gerard Pique.


.png)
0 comments:
Post a Comment