• HABARI MPYA

    Friday, September 07, 2012

    BEKI MAN UNITED ANASWA 'AKIMLA DADAKE' HADHARANI, ASWEKWA LUPANGO


    KINDA wa akademi ya Manchester United, amekamatwa na Polisi kwa tabia chafu ya kufanya ngono na binti anayemzidi umri, tena hadharani.
    Luke McCullough, mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa Nahodha wa akademi hiyo msimu uliopita, alinaswa akimla raha binti huyo mwenye miaka 19 kwenye kamera za CCTV alfajiri ya saa 11:00 Jumatatu baada ya kutokakujirusha.
    Beki huyo wa Ireland Kaskazini, anasifiwa na mabosi wa Old Trafford kuwa 'Jonny Evans mpya'.
    Arrest: Luke McCullough (right) in action for Manchester United's youth team
    Luke McCullough (kulia) akiichezea Manchester United dhidi ya Chelsea

    Tukio hilo lililotokea Concert Square, baa moja maarufu Liverpool, litamchanganya sana Kocha Sir Alex Ferguson, ambaye wiki iliyopita aliwapiga marufuku wachezaji wake wote wa U23 kuendesha magari mapya ya kimichezo kutoka kwa wadhamini wao wapya, Chevrolet.
    Inadaiwa wawili hao walitoka nje ya mlango kidogo na kuvua nguo nusu kisha kuanza kupelekeshana
    Maofisa wa Polisi walipowaona wakawazungukia na kuwakamata. Kabinti kaliachiwa kwanza baada ya kuieleza Polisi ukweli wa tukio, wakati Nahodha wa timu ya vijana ya Ireland, na beki wa kati alishikiliwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa.
    Msemaji wa Jeshi la Polisi Merseyside, alithibitisha kukamatwa kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 na binti mwenye miaka 19 alfajiri ya Jumatatu.

    WASIFU WA LUKE MCCULLOUGH

    • Kuzaliwa: 15/2/1994, Portadown, N. Ire
    • Nafasi: Beki la kati
    • Timu ya taifa: Ireland Kaskazini (U17)
    • Kujiunga United: 1/7/2010
    • Msimu huu: Nahodha Man U Akademi, amecheza mechi 25 
    • Timu za awali: Dungannon Swifts, County Armagh na Portadown Colleg

    Soma zaidi: http://www.dailymail.co.uk
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI MAN UNITED ANASWA 'AKIMLA DADAKE' HADHARANI, ASWEKWA LUPANGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top